Saturday, April 18, 2015


MBEYA CITY na Simba SC zinaingia katika mechi ya leo ya ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa uwanja wa Sokoine zikiwa na matumaini yanayofanana.
Simba wanahitaji pointi tatu zitakazosaidia kuwaweka mazingira mazuri ya kuwania nafasi mbili za juu ambazo zinatoa nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
Pointi tatu ni muhimu kwa Mbeya City ili kuendelea kujihakikishia kubaki ligi kuu msimu ujao, ikumbukwe Mbeya City pamoja na kuwa nafasi ya 10 wakiwa na pointi 25 wanaizidi pointi nne tu Polisi Morogoro inayoshika mkia kwa pointi 21.
Mchezo wa leo ni muhimnu mno kwa wakazi wa Mbeya na mji unaonekana umepoa, lakini wakazi wengi wa jiji hili wana hamu ya kupata matokeo.
Simba wapo kambi ya mafichoni nje kidogo ya jiji la Mbeya na mtandao huu umefika hapo na  kuzungumza na kocha msaidizi Seleman Matola.

JE, SIMBA WAMEJIANDAAJE NA MECHI YA LEO DHIDI YA MBEYA CITY?

Matola anasema: "Tunajua mechi ni ngumu sana, Mbeya City ni timu ngumu inapokuwa nyumbani, lakini tumejiandaa kukabiliana na ugumu wa mechi ya leo kuhakikisha tunatoka na pointi tatu.

MBEYA CITY NI MOJA YA TIMU INAYOKWEPA JANGA LA KUSHUKA DARAJA, SIMBA HAWAONI KAMA NI CHANGAMOTO KWAO KUCHUANA NAYO?

Matola anajibu: "kweli ni changamoto, tunajua mechi haitakuwa rahisi, lakini sisi tumejipanga kukabiliana na mechi ya leo kuhakikisha tunatoka na ushindi"

MATOLA ALICHEZA SIMBA KWA MUDA MREFU NA UWANJA WA SOKOINE ULIKUWA MGUMU KWA SIMBA MPAKA LEO, KILA WANAPOTEMBELEA JIJIJI HAPA WANAHANGAIKA KUPATA MATOKEO, MATOLA ANASEMAJE KUHUSU HILO?

Matola:  "Tatizo siku za nyuma lilikuwa ni uwanja, ujue Simba tunapenda kucheza mpira wa chini na pasi, lakini uwanja ulikuwa hauturuhusu. Kwasasa uwanja unachezeka tofauti na siku za nyuma na kwa falsafa yetu tunaamini tutacheza mpira mzuri"

Hata hivyo Simba inamkosa mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi  ambaye ana kadi tatu za njano pamoja na beki wa kulia Hassan Kessy ambaye wameshamalizana naye mambo yao na kurudi kikosini, lakini hachezi kwasababu hayuko fiti.

VIPI KWA UPANDE WA TIMU MWENYEJI, MBEYA CITY FC?

Kocha mkuu, Juma Mwambusi anasema: "Timu ipo katika hali nzuri, baada ya kurudi kutoka safari tumeshatoa uchovu, tumefanya mazoezi ya mwisho jana kuhakikisha tunajiwinda na mechi yetu ya leo".

KUNA BAADHI YA WACHEZAJI WALIKOSEKANA KWENYE MECHI DHIDI YA YANGA AKIWEMO STEVEN MAZANDA, NAYE THEM FELIX ALIPEWA KADI NYEKUNDU, MAPENGO HAYA YANAIATHIRI VIPI MBEYA CITY KATIKA MECHI YA LEO?

Mwambusi anajibu: "Mimi nasema ni wachezaji muhimu, kwa mfano Themi (Felix) na Steven Mazanda ambaye anaumwa, Mwegane (Yeya) naye anarudirudi, lakini daktari anasema tunaweza kumtumia, kikubwa ni kwamba timu ya Mbeya City imesajili wachezaji zaidi ya 20, wengine watachukua nafasi zao ambao ni majeruhi pamoja na huyo aliyepewa kadi nyekundu ambayo ilitusikitisha, lakini ndio hivyo"

MWAMBUSI ANAWACHULIAJE SIMBA?

Anasema: "Unajua ligi ya mwaka huu ina changamoto sana, Simba ni timu ngumu, manake hii ratiba haikuwa rafiki kwetu, tumetoka Mtwara na Ndanda, tukaenda Dar es salaam kucheza na Yanga na kwa kipindi kifupi leo tunakutana na Simba, sisi tunakubali kwasababu ndio upangaji wa ratiba wa TFF, lakini waangalie sana, bahati nzuri wachezaji wapo katika hali nzuri".

MSIMAMIZI WA KITUO CHA MBEYA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SOKA MBEYA (MREFA) SELEMAN HAROUB ANAZUNGUMZIAJE MAANDALIZI?

"Maandalizi yamefikia katika hatua nzuri kwa maana ya kwamba tumeshaongea na jeshi la polisi kwa ajili ya kuweka usalama kwa timu shiriki,  Mbeya City na Simba"
"Tumeshakamilisha zoezi la tiketi na asubuhi mapema tunaanza kuziuza kwa mashabiki ili waingie uwanjani mapema"

Simba haijawahi kuifunga Mbeya tangu ipande ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita.
Leo ni mara ya nne timu hizi kukutana na mwaka jana katika mechi mbili za msimu, Simba ilitoka sare ya 2-2 na City uwanja wa Taifa na ilipoenda Mbeya ilitoka sare tena ya 1-1.
Msimu huu Mbeya City walianza kwa kuifunga Simba mabao 2-1 uwanja wa Taifa na leo itakuwaje? tusubiri dakika 90'.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video