Saturday, April 18, 2015

Na Kassim Mtolea, Mwanza

TIMU ya soka ya Stand United (Chama la wana) inaondoka hii leo kuelekea jijini Dar es salaam kuwakabili vinara wa ligi kuu ya bara, Dar Young Africans.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Stand United, Muhibu Kanu,timu inaondoka leo  jumamosi tayari kabisa kuivutia kasi timu ya yanga.

Amesema mara baada ya mchezo wao na JKT Ruvu kuisha kwa sare hawana cha kupoteza wanaangalia mchezo dhidi ya Yanga siku ya jumanne.

"Tunaondoka leo jumamosi kuelekea jijini Dar es salaam kucheza na Yanga siku ya jumanne kila kitu kipo sawa na tuna imani na ari kubwa kuelekea huko"
Halikadhalika Kanu amesema kutoa sare katika mchezo wao na Jkt hakuwanyimi furaha kikubwa inawajenga kwenda kupambana na Yanga.
Ameongeza kuwa wao kama timu hawako kwenye ubingwa na wala ubingwa haukuwa kwenye mipango yao kwa msimu huu wao wa kwanza.
"Kama tulivyopanga kabla ya msimu kuanza kwamba malengo yetu ni kuibakisha timu kwenye ligi kuu na sio kutafuta ubingwa,kama tukifanikiwa hilo tutakaa tena kupanga mikakati ya ubingwa msimu ujao"aliiambia MPENJA BLOG.
Stand United inakwenda jijini humo huku ikiwa na kumbukumbu ya kuchezea kichapo cha magoli matatu kutoka kwa Yanga katika mzunguko wa kwanza wa ligi kwa magoli ya Mbrazil Jaja na Jerry Tegete aliyetupia mawili.
Lakini pia watashuka dimba la taifa kwa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kutoka sare ya 1-1 na mnyama Simba uwanjani hapo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video