Mashabiki na wanachama wa timu ya soka ya Simba wa tawi la mpira na maendeleo maarufu kama UKAWA wamepata ajali mkoani Morogoro wakati wakielekea mkoani shinyanga kwenye mchezo kati ya timu ya kagera sugar dhidi ya simba.
Akizungumza na mtandao huu mmoja kati ya mashabiki hao Frank Ngowi amesema ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkundi nje kidogo ya manispaa ya Morogoro imetokana na gari lao kupishana na gari lingine na kisha kupoteza muelekeo.
Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha huku majeruhi zaidi ya kumi hivi sasa wapo hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu.



0 comments:
Post a Comment