Thursday, April 9, 2015

SIMBA SC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Toto African katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10:00 jioni siku ya jumamosi.
Simba imetua Mwanza ikitokea Musoma ilipolala jana ikitokea Roliya Mara ambako ilishiriki bonanza kubwa la michezo ikicheza mechi ya Ndondo na kuzindua tawi la klabu hiyo.
"Mechi ya Toto ni maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya Mgambo uwanja wa Taifa, timu itarejea Dar es salaam kusubiri ratiba iliyopo. Kocha anafurahishwa na programu yetu na ameahidi kufanya vizuri katika mechi tano zilizosalia". Amesema Hajji.
Jumatatu ya wiki hii, Simba ilishinda magoli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Mjini Shinyanga.
Magoli ya Simba siku hiyo yalifungwa na Ramadhan Singano na Abrahim Hajibu kwa mkwaju wa penalti. 
Kagera walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Rashid Mandawa.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video