IBRAHIM Hajibu ni miongoni wa vijana waliojichukulia umaarufu siku za karibuni katika soka la Tanzania.
Nyota huyu kinda wa Simba ni mjanja mjanja wa kuchezea mpira, pasi za visigino, kufunga magoli na kupiga mikwaju ya penalti.
Simba waliifunga Tanzania Prisons 5-0, Hajibu alipiga magoli matatu 'hat trick', moja la penalti. Alipiga penalti kali.
Ana staili yake ya upigaji matuta, anatoka mbali kidogo na mpira, anavuta hatua kama hataki kwenda, anamuangalia kipa na kupiga eneo la juu upande wa kulia au kushoto. Kipa anaiona kabisa, lakini hawezi kuifikia kwasababu anapiga eneo la kutagia kuku yaani kona ya juu.
Jumatatu ya wiki hii, Simba ilishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Magoli yalifungwa na Ramadhan Singano na Ibrahim Hajibu kwa mkwaju wa penalti iliyotokana na jitihada za Singano na Emmanuel Okwi.
Alipiga kwa ufundi wake uleule na kumuacha kipa wa Kagera, Agathon Antony akiwa hana la kufanya. Hakubadili staili yake, alitoka mbali kidogo, alivuta hatua kama hataki, alimuonesha kipa kuwa anapiga upande wa kulia, kipa aliiona, lakini hakuweza kuifikia kwasababu alipiga kwenye kona ya juu kama kawaida yake.
Mtandao huu umemuuliza Hajibu, huwa anabahatisha au anajifunza? naye amejibu;
"Kaka penalti haina mwenyewe, japokuwa kwa asilimia 90 wataalamu wanaamini penalti ni goli,lakini kupiga sio jambo rahisi". Amesema Hajibu na kuongeza,"Mimi sibahatishi, najifunza kupiga penalti mazoezi kwa staili zangu, hii nimefanikiwa, bado nyingi tu zijaonesha, kama tutazidi kupata penalti mechi zajazo, utaona kama nabahatisha au la".

.jpg)
0 comments:
Post a Comment