AMISS Tambwe jana alifunga magoli manne (4) peke yake dhidi ya Coastal Union katika ushindi wa Yanga wa magoli 8-0.
Mabo mengine yalifungwa na Simon Msuva (mawili), Kpah Sherman (moja) na Salum Telela (moja).
Msuva amefikisha mabao 13 na ndiye kinara ufungaji wa magoli akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Azam fc na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar.
Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 43 kileleni baada ya kucheza mechi 20 wakifuatiwa na Azam fc waliopata sare ya 1-1 katika mechi yao ya 19 jana Azam Complex dhidi ya Mbeya City fc na kufikisha pointi 37.
Tambwe baada ya kufunga magoli manne (4) amesema:
"Nimefurahia sana kwa kufunga magoli manne, mshambuliaji yeyote anapenda kufunga. Ligi ni ngumu, wachezaji wanakamia, lakini nikakaa chini na kufanya juhudi zaidi katika mazoezi, angalia nilivyocheza! nitafanya hivyo zaidi katika mechi zilizosalia". Amesema Tambwe.
"Bado mechi zipo, naweza kufunga magoli mengi zaidi, kabla ya mechi ya jana nilikuwa na magoli matano tu, lakini sasa nina magoli 9, hakika ni faraja kwangu na mechi zilizosalia naweza kupindukia kila kitu". Aliongeza Tambwe.

0 comments:
Post a Comment