Thursday, April 9, 2015

KPAH Sherman amefuta mkosi baada ya kufunga goli lake la kwanza katika michuano ya ligi kuu tangu asajiliwe dirisha dogo la usajili desemba mwaka jana.
Goli hilo alifunga jana katika ushindi wa Yanga wa magoli 8-0 dhidi ya JKT Ruvu na baada ya goli hilo, Sherman alimwaga machozi.
Mbuyu Twitwe alimfuata, akapiga goli moja na kunyanyua goti lingeni, Sherman akapandisha mguu wake na kuweka kwenye goti la Twite, halafu Twite akafuta kiatu chake kwa jezi yake.
Mbali na kufunga goli hilo, Sherman alitoa pasi za mwisho za magoli matatu.
Sherman amezungumza na mtandao huu na kueleza:
"Asante sana mashabiki, wachezaji na viongozi wa Yanga kwa kunisapoti kwa muda mrefu, nilikuwa naumia sana kwanini sifungi. Toka nimefika sikuwahi kufunga na nilikuwa nashangaa sana"
"Cha kushangaza kila ninapocheza napata nafasi, angali hata jana nilipata nafasi zaidi ya moja, lakini nikafunga moja. Mchezaji yeyote kuna wakati wa kushindwa na kufanikiwa, nimeshindwa sana, sasa huu ni mwanzo kwangu. Nimefurahi sana na nitaendelea kufanya haya baada ya hapa. Mbali na kufunga, napenda kuisaidia timu kama nilivyofanya kutoa pasi tatu za magoli". Amesema Sherman.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video