Gabon imechaguliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika- CAF- kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017. Nchi hiyo iliandaa michuano hiyo mwaka 2012 kwa kushirikiana na Equatorial Guinea. Gabon itatumia viwanja vinne: Libreville chenye uwezo wa kuchukua mashabiki 45,000, Franceville, mashabiki 25,000, Port Gentil mashabiki 20,000 na Oyem mashabiki 20,000.
Viwanja vya Port Gentil na Oyem bado havijakamilika, lakini afisa kutoka Gabon amemuambia mwandishi wetu Piers Edwards kuwa vitakamilika baada ya miezi 14.


0 comments:
Post a Comment