KWA miaka mitano (5) sasa Simba hawana rekodi ya kupata matokeo mazuri katika mechi za ligi kuu zinazochezwa kandi ya Ziwa (Mwanza na Kagera, na sasa Shinyanga).
Leo jioni majira ya saa 10:00 jioni, Mnyama anachuana na Kagera Sugar katika mechi ya ligi kuu inayochezwa uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.
Kumbukumbu kwenye makitaba ya mtandao huu zinaonesha kuwa kutoka msimu wa 2010/2011 Simba wamecheza mechi nne (4) dhidi ya Kagera Sugar kanda ya ziwa uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.
Katika mechi hizo wameshinda mechi 1, wamefungwa 1 na kutoa sare mechi mbili.
Kwa mara ya mwisho Simba kupata ushindi kanda ya ziwa ni 2010 waliposhinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, Kaitaba, (Oktoba 27, 2010).
Hata kipindi Toto African wapo ligi kuu msimu 2010/2011 mpaka 2012/2013 waliposhuka daraja, Simba ilicheza mechi tatu (3) kanda ya ziwa na kutoka sare zote.
Baada ya Toto kushuka msimu huu Stand United iliwafunga Simba 1-0 uwanja wa CCM Kambarage, februari 22 mwaka huu.
Kutokana na rekodi hizi, mechi ya leo inatabiriwa kuwa ngumu.
Mpira wa sasa wa kisayansi wataalamu wanasema historia haina nafasi, lakini kuna wakati inafanya kazi.
Je, Simba leo watavunja mwiko wa kutoshinda kanda ya ziwa kwa muda mrefu?


0 comments:
Post a Comment