Saturday, April 4, 2015

KATIKA hali isiyotarajiwa uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva umeshindwa kutoa gari kuwarudisha Dar es salaam wanachama wa Tawi la Mpira na Maendeleo 'Simba Ukawa' waliojeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana Mvomero Morogoro wakielekea Shinyanga kuisapoti timu yao dhidi ya Kagera Sugar na kuua watu nane (8).
Akizungumza na mtandao huu mwanachama wa 'Simba Ukawa' ambaye kwasasa ndiye anawauguza wenzake kwa kusaidiana na wengine wenye nguvu japokuwa na yeye ni majeruhi, Frank Ngowi amesema Shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa Costa moja na wao wameagiza ya kwao ije iwachukue Morogoro na kuwarudisha Dar kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo wameshangazwa na kitendo cha viongozi wa Simba kushindwa kutoa gari wakati wao ni Wanasimba wenzao.
Frank amezungumza maneno haya hapa chini muda mfupi uliopita:

"Hakuna huduma yoyote hapa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, kila kitu tunaingia mfukoni. Hivi ninavyokwambia hapa nimeumia mguu na mbavu, nafanyafanya mazoezi kwasababu nikisema nikae huu mguu 'utanichachia', nikisema nilale yaani inakuwa ni shida, yaani hapa hakuna dawa, huduma ni shida".
"Habari za jana ni zilezile, watu wa mpira na Maendeleo waliofariki ni  sita (6) na wengine ndugu zetu wanachama wa Simba ambao tuliwapatia hapa Morogoro  ni wawili kwahiyo watu nane (8) ndio wamefariki".
"Majeruhi mpaka sasa ni watano (5) , wanaendelea vizuri, wanaweza kuongea nao, unaelewana nao na hata chai na maji wanakunywa".
"Wengine wote 15 tuko freshi, tunatembeatembea na kufanya mazoezi".

"Tuombeni kwa Mungu jamani tuwe na afya, lakini kuna ile gari yetu inakuja kutufuata hapa pamoja na nyingine ya TFF. Uongozi wa Simba umeshindwa kutoa gari ya kuturudisha Dar es salaam. Sisi tunazo gari  nne, Costa tatu na Rosa moja". Amesema Frank.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video