Friday, April 3, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Huu ni msimu wa tatu Simba SC inakosekana katika michuano ya kimataifa kutokana na kumaliza nje ya nafasi mbili za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.'

HUKU wakiwa na kibarua kigumu kesho dhidi ya Kagera Sugar FC mjini Shinyanga, kocha mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic, amekiri kichwa chake kinauma anapozifikiria pointi 18 za mechi zao sita zilizobaki kabla ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC, mabingwa mara 18 wa Tanzania Bara, watakuwa na kazi ngumu ya kupata pointi dhidi ya kikosi shadidi cha Kagera Sugar katika mechi yao ya kesho usukumani Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Katika mahojiano na mtandao huu akiwa mjini Shinyanga muda mfupi uliopita, Hajji Manara, msemaji wa Simba SC, amesema kuwa Kopunovic amewakumbusha nyota wao kuhusu umuhimu wa kuchukua pointi zote 18 katika mechi sita zilizosalia kabla ya kumalizika kwa msimu Mei 9, mwaka huu.

Manara, mtoto wa nyota wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara, amesema kuwa jana kikosi chao kilijifua Uwanja wa Shule ya Sekondari Com mjini humo na leo kinafanya mazoezi Uwanja wa CCM Kambarage kujiweka sawa kabla ya kukikabili kikosi cha Mganda Jackson Mayanja ambacho kimepoteza mechi moja tu kwenye uwanja huo tangu kihamishie maskani yake mjini Shinyanga kikitokea Mwanza miezi miwili iliyopita.

"Kocha mkuu (Kopunovic) amekumbusha kuhusu umuhimu wa kupata pointi zote 18 katika mechi zilizobaki maana ndizo zitakazotupa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani," amesema Manara.

Kikosi cha Simba SC chenye wachezaji 24 kilitua mjini Shinyanga juzi usiku bali beki wake mahiri wa pembeni kulia, Hassan Kessy, ambaye ameamua kujiweka pembeni mwa timu hiyo ya Msimbazi kwa madai ya kutotimiziwa matakwa ya kimkataba na uongozi.

Kagera Sugar FC, mabingwa wa Kombe la Tusker 2004, waliifunga Simba SC bao 1-0 Uwanja wa Taifa jijini hapa Novemba mwaka jana. Shukrani kwa bao la Atupele Green lililokumbusha uchungu wa sare ya 1-1 ya msimu uliopita wa ligi iliyowachefua baadhi ya mashabiki wa Simba SC waliokwaza na refa Mohamed Teofile wa Morogoro baada ya kuipa tuta la dakika za mwisho lililopia sare timu hiyo ya Kagera.

Baada ya kucheza mechi 20, Simba iko nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32, nane nyuma ya vinara Yanga SC na tano mbele ya Kagera Sugar FC walioko nafasi ya nne baada ya mechi 20 pia.

Mechi 6 za Simba zilizobaki ni:
Kagera Sugar FC    vs    Simba SC
Simba SC    vs Mgambo Shooting Stars
Mbeya City FC    vs Simba SC
Simba SC vs Ndanda FC
Simba SC vs Azam FC
JKT Ruvu vs Simba SC

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video