
Manuel Pellegrini amekiri kuwa amefadhaishwa sana na Yaya Toure lakini ameahidi kumpa 'sapoti' kiungo huyo mpaka pale msimu utakapokuwa umemalizika.
Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Man City ipo tayari kusikiliza ofa ya Toure kutoka klabu yoyote ile huku wakiwa katika harakati ya kusafisha kikosi chao hasa kwa wachezaji wote wanaoonekana kuwa umri umewatupa mkono.
Toure inasemekana hatalazimishwa kuondoka na kocha huyo, akiongea wakati wa maandalizi ya mchezo wao wa Jumapili dhidi ya West Ham, Pellegrini amekiri kuwa kiungo huyo raia wa Ivory Coast amekuwa chini ya kiwango katika siku za hivi karibuni huku akikanusha taarifa za kupewa mapumziko kwa kiungo huyo.
‘Sidhani kama hata yeye pia ana furaha kwa kiwango alichokionesha mwaka huu — na hata mimi sina pia,’ Pellegrini alisema. ‘hahitaji pumziko lolote lile.’
Toure, ambaye amebakisha miaka miwili tu katika mkataba wake na Man City ambao unamfanya apokee kiasi cha Paundi 220,000 kwa wiki, amekuwa akikosolewa katika baadhi ya mechi ambazo City imecheza hovyo hasa safu ya ulinzi. Lakini Pellegrini, ambaye kuna uvumi mwingi kuhusu kuendelea kuwepo klabuni hapo, amesema Toure lazima tu atarudi katika hali yake ya kwaida.
‘Ni mchezaji muhimu sana na nitaendelea kumuunga mkono daima mpaka mwisho wa msimu,’ alisema Pellegrini.

0 comments:
Post a Comment