Harry Kane ana thamani ya Pauni Milioni 100 kwa mujibu wa Straika wa zamani wa England Rodney Marsh.
Kinda huyo wa Miaka 21 ameibuka Msimu
huu na kuifungia Klabu yake Tottenham Mabao 29 na Ijumaa iliyopita,
akiichezea England kwa mara ya kwanza kabisa, alifunga Bao lake la
kwanza Sekunde 79 tu tangu aingizwe kutoka Benchi.
Rodney Marsh, ambae aliichezea England
mara 9, amesema: "Thamani yake sasa ni Pauni Milioni 100. Nadhani
atapanda na kuwa bora kupita Alan Shearer,Man City ililipa Pauni
Milioni 32 kumnunua Mchezaji asiejulikana Eliaquim Mangala. Ikiwa
Mangala thamani yake ni Pauni Milioni 32, Harry Kane ni lazima thamani
yake ni Pauni Milioni 100!"
Aliongeza: "Angel Di Maria ameigharimu Man United Pauni Milioni 60. Nadhani Harry Kane ni Mchezaji bora kupita Di Maria!"
0 comments:
Post a Comment