Wakati Marouane Fellaini akiipa ushindi Belgium na kutwaa uongozi wa
Kundi B la EURO 2016, Portugal walitandikwa kwao 2-0 na Kinchi kidogo
Visiwa vya Cape Verde ambao ni Koloni lao la zamani.
Belgium, wakicheza Ugenini, waliichapa Israel 1-0 na kushika uongozi wa Kundi B juu ya Wales ambao wanafungana nao kwa Pointi,Bao la ushindi la Belgium lilifungwa Dakika ya 9 na Mchezaji wa Man
United Marouane Fellaini lakini walimaliza Mechi hiyo Mtu 10 baada ya
Beki wa Man City Vincent Kompany kutoĺewa nje kwa Kadi Nyekundu katika
Dakika ya 64 kufuatia Kadi za Njano 2,baada ya mchezo huo sasa mechi inayofuata kwa Belgium ni ugenini dhidi ya Wales.
Nayo timu ya taifa ya Portugal ikicheza nyumbani bila Mchezaji wao Bora Duniani Cristiano Ronaldo ilipigwa bao 2-0 na Timu ndogo ya Afrika Cape Verde,mabao ya Cape Verde yalifungwa na wachezaji mahiri Fortes na Estalline Dias Barros.
0 comments:
Post a Comment