Thursday, April 2, 2015



Na Bertha Lumala, Shinyanga
Mandawa weka mbali na watoto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya straika huyo hatari Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kuiongoza timu yake ya Kagera Sugar FC kupeleka maangamizi Manungu kwa kuichapa Mtibwa Sugar FC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini hapa jioni hii.

Mechi hiyo pekee ya leo ya Ligi Kuu Bara imechezwa huku kukinyesha mvua mjini Shinyanga, lakini haikuwazuia wakatamiwa wa Kagera kuwasambaratisha ndugu zao.

Kwa ushindi huo wa nne tangu ihamishie maskani Shinyanga miezi miwili iliyopita, Kagera Sugar FC, ambayo itacheza dhidi ya Simba SC Jumamosi, imeendelea kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikifikisha pointi 27 baada ya mechi 20 wakati Mtibwa Sugar FC imeendelea kusalia nafasi ya saba ikiwa na pointi 23 baada ya mechi 19.

Kikosi cha kocha mkuu Mganda Jackson Mayanja cha wenyeji Kagera Sugar FC kilipata bao lao la kwanza kutokana na krosi kali ya Malegesi Mwangwa iliyowababatiza kipa pamoja na beki wa pembeni na nahodha wa Mtibwa Sugar FC, Said Mkopi dakika nne kabla ya nusu saa ya mchezo.
 
Dakika moja kabla ya mapumziko, Ame Ally Amour, mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu ya Zanzibar, ameifungia Mtibwa Sugar FC bao akiunganisga kwa shuti kali la mguu wa kulia pasi safi ya Mkopi na kuzifanya timu hizo zipumzike zikiwa sare ya 1-1.
 
Lilikuwa bao la saba kwa mshambuliaji huyo msimu huu sawa na Abasirim Chidiebere wa Stand United FC, Emmanuel Okwi wa Simba SC na Samwel Kamuntu wa JKT Ruvu Stars.

Mandawa, mmoja wa washambuliaji hatari Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ameipatia Kagera Sugar FC bao la ushindi likiwa ni bao lake la tisa msimu huu, mawili nyuma ya kinara Simon Msuva wa Yanga SC na moja nyuma ya Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC anayeshikilia nafasi ya pili kwa wafumania nyavu hatari msimu huu.

Kikosi cha Mtibwa Sugar FC kitaendelea kupiga kambi mjini Shinyanga kikisubiri kucheza dhidi ya wenyeji Stand United FC Jumapili wakati Kagera Sugar itaivaa Simba SC mjini humo Jumamosi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video