YANGA wanakwea pipa leo usiku kuwafuata Etoile du Sahel kucheza mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho.
Mechi ya kwanza jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, hivyo Yanga wanahitaji ushindi au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ameuambia mtandao huu jioni hii kuwa kikosi cha Yanga kitaondoka na Ndege ya biashara ya Emirates majira ya saa 4:25 usiku na kitapitia Dubai.
"Vijana wanaondoka leo usiku saa 4:25 na ndege ya Emirates kupitia Dubai". Amesema Muro na kusema: "Vijana wana morali, mimi nakwambia lazima jamaa (Etoile) waloe, unajua hakuna kitu kibaya kama watu dhaifu kujipanga na kucheza kama siafu, wanakuwa na nguvu kubwa, wao wanajiona wana mpira mkubwa sana, watacheza kwa kujiamini, sisi tutashambulia"
"Wakikaa mara mbili tu watalala, uwezekano wa kuondoka na ushindi ni mkubwa sana. Babu ( kocha Hans van der Pluijm) ana matumaini makubwa sana na kikosi chake, ana imani ya vijana wake kufanya vizuri".
0 comments:
Post a Comment