Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akikabidhiwa mpira na mwamuzi wa mchezo wa jana kati ya Simba na Mgambo JKT katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kufunga mabao matatu (3) (hat-trick) peke yake kati mabao 4 ambayo timu yake iliibuka nayo.
Mashabiki wa Simba wakiufuatilia mchezo wakati timu yao ilipokuwa ikipepetana na Mgambo JKT hapo jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu yao iliibuka na ushindi wa mabo 4-0.
Waamuzi wakigakua nyavu za magoli kama zipo salama tayari kwa mtanange
Vijana waokota mipira uwanjani (ball boys) wakisaidiana kukamua taulo la mlinda mlango wa Simba Ivo Mapunda
Ivo Mapunda akikabidhiwa taulo lake baada ya kukamuliwa kutokana na kuloa kulikosababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo
Okwi akikabidhiwa tunguli na mshabiki wa Simba kama shukrani baada ya kuifungia timu yao magoli matatu kati ya manne ambayo timu yao iliweka kimiani.
0 comments:
Post a Comment