Vijana waokota mipira, 'Ball Boys' wakikamua taulo la Ivo
IVO Mapunda ni miongoni mwa makipa waliopitia
misukosuko mingi katika klabu za Simba na Yanga.
Kabla ya kuichezea Simba, Ivo alikuwa kipa mahiri
ndani ya klabu ya Yanga na Taifa Stars, lakini alikuwa anatuhumiwa mara kadhaa
kuihujumu timu na kushuka kiwango.
Ikafika wakati akaona isiwe taabu! akatimkia Ethiopia
katika klabu ya Saint George na alicheza kwa mafanikio. Amepitia sehemu nyingi,
lakini mwaka jana kabla ya kuja Simba alikuwa kipa muhimu kwenye kikosi cha Gor
Mahia ya Kenya.
Kipa huyu ni mahiri kudaka penalti na kila
ilipofikia hatua hiyo, Gor Mahia walimuingiza kuokoa jahazi na alifanya hivyo.

Kijana akimpatia Ivo taulo baada ya kulikamua
Aliposajiliwa na Simba amekuwa akicheza vizuri,
kuna wakati anafanya makosa ya kimchezo, lakini watu wanazungumza vibaya.
Lakini cha kufurahisha ni kwamba Ivo kamwe hakati tamaa
na muda wote anajituma, anajua kukubali changamoto na kupotezea maneno ya watu.
Jana aliidakia Simba baada ya kukosa mechi tatu
kutokana na kupewa kadi nyekundu machi 18 mwaka huu Simba ikilala 2-0 dhidi ya
Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Ilikosa mechi dhidi ya Ruvu Shootings Simba
ikishinda 3-0, akakosa mechi na Kagera Sugar Mnyama akishinda 2-1 na mechi ya
mwisho ni ile Simba waliyolala 2-0 dhidi ya Mbeya City.
Akiwa kwenye kiwango kikubwa, Ivo mwenye tabia ya
kuwa na taulo kubwa golini jana alikumbwa na tatizo na nguo yake hiyo ya
kufutia jasho ingawa wapinzani wanaitafsiri vibaya.
Taulo lilijaa maji, lakini vijana wanaookota
mipira, ‘Ball Boys’ kwa mapenzi yao walilichukua taulo na kuanza kulikamua
maji.
Walifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa na
kumkabidhi Ivo, ilikuwa burudani nzuri sana.
0 comments:
Post a Comment