Thursday, April 23, 2015

Nahodha wa zamani wa Arsenal na nguli wa klabu hiyo Thierry Henry amekosoa kitendo cha mshambuliaji wa Real Madrid Javier Hernandez kwa kitendo chake cha kutoonesha shukrani kwa Ronaldo mara baada ya kumpa pasi ambayo ilizaa bao pekee katika mchezo wa jana wa klabu bingwa dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid uliopigwa jatika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Chicharito ambaye yupo Madrid kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester United alifunga bao hilo kwa umaridadi baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ronaldo.
Henry ameshutumu kitendo cha Chicharito kushangilia kwa namna ile na kusema kuwa“Inakuwa kama vile ameshinda kombe la dunia” na kusisitiza kuwa angetakiwa kumshukuru Ronaldo kwa kumfuata na kumkumbatia kama ishara ya shukrani kwa alichokifanya.
"Hata hivyo sijui kama ataendelea kuwepo pale. kusema tu ukweli ni kwamba kwanza mara nyingi huwa hapati nafasi ya kucheza. Jana ndiyo ilikuwa siku ya pekee kuapata fursa ile na hatuhjui hata kama atapata tena nafasi ya kuendelea kuwepo pale,” Henry aliiambia Sky Sports.
“Alipata nafasi nyingi sana za kufunga lakini alishindwa kuzitumia, lakini nakwambaia ni lazima tu amshukuru Ronaldo.
“Kwangu mimi hilo goli nampa Ronaldo. Kitu ambacho sikufurahishwa nacho ni kwamba baada ya kufunga goli lile alionekana kama vile ameshinda kombe la dunia, badala ya kugeuka na kushangilia pamoja na Ronaldo kama ishara ya kumshukuru kwa pasi nzuri aliyompa."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video