Thursday, April 2, 2015


Na Bertha Lumala
Uzee dawa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Yanga SC kuwazuga wapinzani wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, FC Platinum kwamba wangelienda mapema nchini Zimbabwe kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi ilhali si kweli.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania waliosalia katika michuano ya kimataifa mwaka huu, wamefuta mpango wao wa kutinga mapema nchini Zimbabwe na sasa watawasili nchini humo siku moja kabla ya mechi yao dhidi ya Platinum FC ili kukwepa fitina.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro, alisema Jumapili kuwa kikosi chao kilitarajiwa kwenda Zimbabwe leo asubuhi, lakini imeshindikana na kutokana na kile kilichoelezwa na Bakili Makele kwamba wamebaini timu itakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanyiwa fitina ikiwasili mapema nchini humo.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Vijana wa Yanga SC jiji Dar es Salaam leo kuwa wamelazimika kipangua ratiba yao ya kuwasili Zimbabwe ili kuzikwepa mbinu chafu za wapinzani wao.

"Wapinzani wetu wanasaka kila mbinu ili watufunga mabao mengi nyumbani kwao. Mpaka sasa tumekwepa mbinu chafu tatu. Tumeamua timu isiende Zimbabwe leo ili kukwepa fitina zao ambazo tumejuzwa na watu wetu waliotangulia huko. Timu itaondoka Ijumaa kwa ndege maalum kutoka hapa Tanzania," amesema Makele.

"Yanga ni timu kubwa, hatuwezi kwenda sehemu kichwa kichwa, lazima tuwachanganye wapinzani wetu," amesema zaidi Makele.

Timu ya Yanga SC chini ya kocha mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Boniface Mkwasa, imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa saa moja jana kuanzia saa tatu asubuhi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video