Saturday, April 4, 2015

Kessy (kulia) anaikosa mechi ya leo wakati muuaji wa Simba mwaka jana Atupele Green akitarajiwa kuiongoza tena timu yake leo jioni kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

LIGI kuu soka Tanzania bara inaendeleo leo kwa mechi kadhaa kupigwa viwanja mbalimbali nchini.
Kagera Sugar wanashuka dimbani kuwakaribisha Simba katika mechi ya raundi ya pili ya ligi kuu uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Katika mechi ya leo, Simba inamkosa beki wake mahiri wa kulia, Hassan Kessy Ramadhani aliyeamua kujiondoa kikosini baada ya kutolipwa haki zake na viongozi wa Simba.
Kessy hakusafiri kabisa na timu na yuko kwao mkoani Morogoro.
Masoud Nassor 'Cholo' anatarajia kuziba nafasi hiyo na itakuwa mechi yake ya pili mwaka huu kwani mechi zote 12 alizoongoza Goran Kopunovic, beki huyo mkongwe kutoka Zanzibar alicheza moja tu Simba ikifungwa 2-1 na Mbeya City.
Hii ilikuwa januari 28 mwaka huu uwanja wa Taifa na sababu ya Kessy kukosa mechi hiyo ilikuwa ni kadi tatu za njano.
Mechi nyingine ngumu itakuwa huko Nangwanda Sijaona Wenyeji Ndanda fc wakiikaribisha Mbeya City fc.
Coastal Union wanachuana na Tanzania Prisons katika uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mechi nyingine inachezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani. wenyeji Ruvu Shootings wakikabiliana na ndugu zao wa JKT Ruvu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili zitakazowakutanisha Stand United na Mtibwa Sugar uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Nyingine itashuhudiwa uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo Mgambo watachuana vikali na Mgambo JKT.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video