Saturday, April 4, 2015


Mechi ya kwanza Dar es salaam Yanga walishinda 5-1

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Dar Young Africans leo jioni kuanzia majira ya saa 10:00 kwa saa za Tanzania, saa 9:00 alasiri kwa saa za Zimbabwe wanaikabili FC Platinum katika mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho inayopigwa uwanja wa Mandava.
Mechi ya kwanza ilipigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam februari 15 mwaka huu na kushuhudia Yanga ikishinda mabao 5-1.
Ili kusonga mbele, Yanga inahitaji sare ya aina yoyote, ushindi au kutofungwa zaidi ya magoli manne ambayo yafanya wastani kuwa 5-5 na kuipa FC Platinum faida ya kusonga mbele kwa faida ya ugenini.
Licha ya Yanga kuwa na hazina ya magoli mengi, bado chochote kinaweza kutokea katika mpira.
Wazimbabwe wanaweza kufunga magoli mengi kama wao walivyofungwa Dar es salaam, lakini kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga, tunaamini haitakuwa rahisi.
Kitu cha msingi kwa Yanga ni kuwa na nidhamu ya mchezo hususani dakika 15 hadi 20 za kwanza.
FC Platinum kwa dakika zote watashambulia lango la Yanga kwasababu hawana cha kupoteza na wana mzigo mzito mno, hivyo Yanga itabidi waongezea ulinzi sehemu ya kiungo na kufanya mashambulizi.
Njia nzuri ya kujilinda ni kushambulia, sishauri Yanga wapaki basi hata kidogo.
Kama Yanga watashambulia na kujilinda vizuri, lazima Platinum watakuwa na tahadhari ya kwenda mbele zaidi na watapaniki kadri muda unavyozidi kwenda.
Wanajangwani wanatakiwa kutafuta bao la mapema na kama watafunga hata moja, utakuwa mwisho wa Platinum kwani watakuwa watoka mchezoni kwa asilimia zote.
Najua zinaweza kutokea fitina uwanjani, kubebwa kwa wenyeji kwasababu siku hizi mpira umekuwa na mipango mingi ya uwanjani.
Yanga wanachotakiwa ni kubaki katika nidhamu ya mchezo, kila watakachofanyiwa uwanjani wachukulie ni changamoto, lakini wakianza kuwaza kama wanaonewa, itawafanya wapinzani washinde kwa mbinu zao.
Mabeki wasifanye masihara, wasiwaruhusu na kuwapa nafasi washambuliaji kufika eneo la hatari na kutengeneza mazingira ya kufanyiwa faulo, wawaweke mbali na ukingo wa mita 18 ili kama muamuzi wa mechi itatoa adhabu iwe mbali na golini.
Kocha Hans van der Pluijm anajiamini sana na hatuna wasiwasi na uwezo wake. Lazima ataanza na viungo wengi ili kuwafanya Platinum wasitengeneze mashambulizi kutokea katikati au pembeni ya uwanja.
Binafsi naamini Yanga wanasonga mbele kwa vyovyote vile.
Kila la kheri Yanga katika mechi yenu. Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Tanzania.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video