UKURASA wa facebook wa Naipenda YANGA leo umeandika:
“Sasa ni muda wangu wa kufunga, nimejiuliza sana kwa nini nilikuwa sifungi, lakini nimeshapata jibu, ndiyo maana unaona nafunga, sitaishia hapa nasema huu ndiyo mwanzo, nitazidi kuifungia Yanga katika kila mechi nitakayocheza hata jumapili niliona bora nitoke ili nisije kujiumiza zaidi na nikawakosa Etoile du sahel” alisema Sherman.
Wakati Sherman akifurahia kiwango chake cha sasa ,kiungo aliyetoka majeruhi Andrey Coutinho anaonekana kuwa na mashaka kama ataweza kurudi kikosi cha kwanza kwani anaona ushindani ni mkubwa na timu yote ipo katika fomu ya juu. .
“Kwa sasa nipo fiti kabisa kuweza kurejea uwanjani na kuendelea kucheza kama ilivyokuwa hapo awali na nimejipanga vya kutosha kuhakikisha napambania namba yangu katika kikosi cha kwanza.
“Najua itakuwa siyo rahisi kutokana na viwango ambavyo vinaonyeshwa na wachezaji waliopo kama Msuva na Ngassa lakini nitapambana mpaka mwisho.”alimalizia Andrey Coutinho.


0 comments:
Post a Comment