Chelsea na Manchester United zitakutana kesho Stamford
Bridge kuchuana katika mechi ya ligi kuu England inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki
wengi duniani.
Man United wataingia katika mechi hiyo wakiwa na rekodi
nzuri ya kushinda mechi sita, lakini wachezaji muhimu watakosekana katika
kikosi cha kocha Mholanzi, Louis van Gaal.
Wayne Rooney atalazimika kurudi zaidi katika majukumu ya kiungo
baada ya Michael Carrick na Daley Blind kuondolewa katika kikosi kitakachovaana
na vinara wa ligi guu, Chelsea.
Pia mlinzi wa kati Phil Jones na Marcos Rojo wataikosa mechi
hiyo , Jonny Evans anamalizia adhabu
yake ya kufungiwa mechi sita na tayari Van Gaal ameshaanza kuonesha wasiwasi
baada ya kueleza kuwa yupo katika mazingira magumu kwa kuwakosa wachezaji hao
muhimu.
Jones na Blind walijeruhiwa na Vicent Kompany kwenye mechi ya
mahasimu wawili wa jiji la Manchester, Manchester United na Manchester City.


0 comments:
Post a Comment