Chama kinachopinga ubaguzi wa rangi England ‘Kick It Out’ kimeeleza kuwa kati ya
jumbe elfu arobaini za matusi zinazochapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu
wachezaji wa ligi kuu England zinahusu ubaguzi wa rangi.
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ndiye mchezaji
anayetukanwa kwa zaidi ya jumbe elfu
nane akifuatiwa na Daniel Sturridge na mchezaji wa Arsenal Danny Welbeck na nusu
ya jumbe hizo zinaonesha ubaguzi wa Rangi.
Mkurugenzi wa chama hicho, Roisin Wood amekiri kuongeze kwa
vitendo vya matusi na kueleza kuwa wanaendelea kijidhatiti kupigania haki za
watu wanaobagulia na sasa wanajipanga kupata wawakilishi kutoka katika klabu
zote, mitandao ya kijamii na polisi kwa lengo la kudhibiti matusi hayo hususani
kwenye mtandao wa Twita.


0 comments:
Post a Comment