Friday, April 10, 2015


KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake, Twiga Stars,  Rogasian Kaijage na nahodha wake Sophia Mwasikili, wamewahakikishia Watanzania ushindi katika mchezo wa leo wa marudiano kuwania kufuzu michezo ya Afrika  dhidi ya Zambia na kuwaomba mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwashangilia.


Mechi inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na tiketi za mchezo zitauzwa leo saa 2 asubuhi eneo la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku viingilio vya mchezo huo vikiwa ni tsh. 5000 kwa VIP na tsh. 2000 kwa majukwaa yaliyobakia.



Twiga Stars ambayo katika mchezo wa awali iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanyika nchini Congo-Brazzavile mwezi Septemba.
Mechi ya leo itarushwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video