Friday, April 3, 2015


STRAIKA wa Azam, Didier Kavumbagu amefurahia ushindani ulioletwa na mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva kwa kufunga mabao 11 moja zaidi ya mabao yake 10 lakini ametahadharisha kuwa bao hilo haliwezi kuzima ndoto zake za kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.
Kavumbagu ambaye mkataba wake na Azam unamalizika mapema mwezi ujao alisema kwa sasa ameweka mambo ya kusaini mkataba mpya kando, akili yake ipo katika kuhakikisha Azam inatetea taji ililolitwaa mara ya kwanza msimu uliopita.
Straika huyo wa zamani wa Yanga aliongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara tangu kuanza kwa msimu Septemba mwaka jana mpaka katikati ya juma lililopita ambapo Msuva alifunga mabao mawili na kumpiku.
“Bao moja si kitu, bado tuna mechi tisa zilizobaki, sitacheza moja kwa sababu nina kadi tatu za njano lakini nitazitumia nyingine vilivyo kuweka hesabu zangu sawa, Msuva kaongeza ushindani tu,” alisema raia huyo wa Burundi.
“Masuala ya mkataba nimeyaweka kando kwa sasa, wacha miguu ifanye kazi yake na hayo yatakwenda vizuri msimu ukimalizika,” aliongeza Kavumbagu.
Mpaka sasa Kavumbagu amekuwa na rekodi ya kipekee ya kufunga mabao 10 ama zaidi kwa misimu mitatu mfululizo ambapo aliifungia Yanga mabao 10 katika msimu wake wa kwanza na kisha 11 katika msimu wake wa pili kabla ya kuifungia Azam mabao hayo mpaka sasa.
Source: Mwanaspoti

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video