Manchester United iko katika hatua za mwisho kumnasa mshambuliaji wa kibrazil anaekipiga katika klabu ya Hoffenheim ya Ujerumani,Roberto Firmino ambaye wiki iliyopita alifunga bao la ushindi katika pambano la kirafiki kati ya Brazil na Ufaransa jijini Paris.
Manchester United imekuwa ikimsaka mbrazil huyo kwa muda mrefu sasa na hivi karibuni mmoja kati ya mabosi wa manchester united alionekana akiwa amekaa na Firmino katika pambano moja la ligi kuu ya England.
kuwasili kwa mchezaji huyo katika dimba la old trafford kutahitimisha zama za mshambuliaji Radamel Falcao ambaye amechemsha katika kipindi chake cha mkopo akitokea Monaco kwa dili la Pauni 6 milioni Agosti mwaka Jana, licha ya Falcao kuchemka, klabu mbalimbali za Ligi Kuu England zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili na yeye mwenyewe anasema anapenda kubaki England.




0 comments:
Post a Comment