MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Angel di Maria kwa muda mrefu amekuwa chini ya kiwango tofauti na thamani yake, huku Wayne Rooney akionekana kuwa na msaada katika kikosi cha Loius van Gaal.

Juzi kwenye mechi ya ligi, Di Maria alitolewa wakati wa mapumziko kutokana na kiwango kibovu alichoonesha. Lilikuwa pigo kwa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa paundi takribani 60 kutokea Real Madrid.
Van Gaal anasisitiza kuwa Di Maria anahitaji muda kuzoe ligi kuu England, lakini kumekuwa na dukuduku kwa namna anavyocheza hasa jinsi alivyoonesha mchango mdogo katika ushindi dhidi ya Sundeland ukilinganisha na thamani yake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid yupo kwenye kiwango cha chini akiwa na Manchester United
Hata hivyo, Wayne Rooney hana wasiwasi kabisa, anaamini mchezaji huyo ana kitu cha zaida na muda si mrefu atapata mafanikio katika ligi ya England.
"Kiukweli hajawa kwenye kiwango," Alisema nahodha wa United. "Kinachomtokea humkuta mchezaji yeyote yule. Muda si mrefu atarudi kwenye moto wake".
0 comments:
Post a Comment