MSHAMBULIAJI hatari wa Real Madrid na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 30 msimu huu, lakini hakufanikiwa kuizuia Real kupata sare ya 1-1 dhidi ya Villarreal katika mechi ya ligi jana.

Goli hilo alifunga kwa mkwaju wa penalti.
Ronaldo amebakiwa na mechi 12 mkononi na tayari ameweka rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga magoli 30 katika misimu minne mfululizo katika moja ya ligi za juu barani Ulaya.
Lakini aliuacha uwanja ukiwa umenuna baada ya Real kushindwa kuwatoa Barca kileleni.
Wapinzani au mahasimu hao wa soka la Hispania wanatofautiana kwa pointi mbili na baadaye mwezi huu, Real watatua Camp Nou kuwafuata Barca.

Gerarda Moreno wa Villareal akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake
0 comments:
Post a Comment