Nyota Harry Kane akiwashukuru mashabiki wa Tottenham wakati wachezaji wa Chelsea wanashangilia ushindi nyuma yake baada ya kushinda 2-0 katika mechi ya fainali ya kombe la ligi

Roberto Soldado alikuwa na nafasi ndogo ya kuisaidia timu na hapa amezungukwa na wachezaji wa Chelsea waliokuwa na furaha

Mchezaji wa Tottenham, Christian Eriksen akiwa amejishika mikono kiunoni baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa na Tottenham ipo nyuma kwa mabao 2-0

Nyuma yake Chelsea wanashangilia ushindi, Mousa Dembele akibaki ameduwaa tu baaada ya Spurs kula kipigo

Danny Rose akiwa amekaa kwa huzuni uwanjani Wembley
0 comments:
Post a Comment