Monday, March 2, 2015

Yassin akifanya mazoezi

BEKI kijana wa kushoto wa 'Chama la Wana', Stand United, Yassin Mustapha ni muoga mno! anaogopa magonjwa ya zinaa 'hakunaga'.
Katika mahojiano maalumu na MPENJA BLOG, Yassin aliyetiwa umeme (kadi nyekundu) Stand 
ikiifunga Simba bao 1-0, uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga amesema ana miaka minne katika mahusiano ya kimapenzi na hapendi michepuko.
Licha ya kuwa mkali wa mahaba, Yassin kuna kitu kimoja tu kimemshinda, nini..hicho, kuhusu simu..soma ujue ni kwanini.
Pia amesema anapenda sana kuzichezea timu kubwa za Tanzania, Simba, Yanga na Azam, lakini ndoto kubwa ni kutua Azam Complex, Chamazi.
Yapo mengi aliyozungumza, ya kimpira na nje ya mpira, fuatilia mahojiano haya hapa chini upate kujifunza na kuburudika;
SWALI: Kwanini hupendi michepuko na umekaa kwa muda gani katika mahusiano yako ya kimapenzi?

Yassin: Aaaah! unajua mimi mtoto wa kiislamu, naijua dini vizuri. Nina nidhamu sana na maisha! michepuko sio dili, sipendi kabisa michepuko kwasababu kubwa moja, kuna magonjwa mengi. Kubwa zaidi, tunaoneshana mapenzi  makubwa mno na mpenzi wangu ambaye nimedumu naye kwa miaka minne. Siwezi kumuacha na sina mpango huo kabisa! nampenda mno!.

SWALI:Wazazi wako walikuunga mkono ulipoanza kucheza soka?

Yassin: Wazazi nao wanakuwa na mambo yao wanayopenda, ujue wao wanaamini sana kwenye masomo. Sio kwamba sitaki kusoma, kuna muda nimejipangia, miaka kadhaa nitacheza soka na baada ya hapo nitarudi Darasani. Nimejiwekea miaka mitatu ya soka kwanza.
Mwanzoni wazazi hawakuniunga mkono moja kwa moja kwasababu walikuwa wanaona hakuna faida yoyote, ila baadaye wakaona mafanikio japo sio makubwa.

Yassin Mustapha (wa pili kulia waliopiga magoti) akiwa kwenye moja ya kikosi cha Stand United

SWALI: Kwanini unapenda sana WatsApp na unawachukuliaje watu wanaokutumia picha mbaya?

Yassin: WatsApp naipenda kwasababu naitumia muda mwingi kutumiana video za soka na marafiki zangu, lakini kiukweli namchukia sana mtu anayenitumia picha za ajabu kwasababu sizipendi.

SWALI: Timu gani umewahi kucheza huko nyuma?

Yassin: Nilicheza Polisi Dodoma tangu nikiwa shule, timu hii ilinikuza na kunipa nafasi ya kuonekana. Pia nimecheza timu ya taifa ya vijana ikiwa chini ya kocha Poulsen (Kim).

SWALI: Mchezaji gani anakuvutia Tanzania?

Yassin: Kwa upande wa nafasi yangu, nampenda sana Mohammed Hussein 'Tshabalala' anayekipiga Simba Sc. Ni mchezaji mzuri, anajua kuchezea mpira, anakaba vizuri na kupandisha timu kushambulia.

SWALI: Mnashirikiana simu za mkononi na mpenzi wako?

Yassin: !oooooh! patamu hapo! kiukweli hapana! hatuna utaratibu huo, sisi tumepanga hivyo, hakuna haja ya ku-share simu. Lakini kama anataka ya kwangu ili aangalie kitu fulani, nampatia.

SWALI: Timu gani unaipenda zaidi Bongo?

Yassin: Napenda nije kupata nafasi katika timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc. Lakini Azam inanivutia zaidi kwa namna inavyoendeshwa, uwekezaji wake, naamini pale unaweza kucheza mpira.

SWALI: Kwa nafasi yako, winga gani aliwahi kukupa shida zaidi?

Yassin: Kipre Tchetche, yule jamaa ni mchezaji wa kiwango cha juu! hahahah alinitoa jasho sana na nilipata shida mno kumkubwa haijawi kutokea!.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video