POLISI FC ya Zanzibar imetupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho kwa kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 8-1 kutoka kwa CF Mounana ya Gabon.
Mounana iliyoanzishwa miaka nane iliyopita (2006) imeinyuka Polisi 3-1 katika mechi ya marudiano iliyopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar jioni ya leo.
Mechi ya kwanza nchini Gabon, Mounana walishinda 5-0 na ushindi wa leo umewafanya wafikisha wastani wa mabao 8-1 na kusonga mbele hatua ya makundi.
Kutolewa kwa Polisi kumeiacha Tanzania iwe na timu moja tu katika michuano ya kimataifa, Dar Yaoung Africans.
Yanga wamefuzu kucheza raundi ya kwanza baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana.
Walishinda 2-0 Dar es salaam, wakapigwa 2-1 Gaborone, wastani wa magoli 3-2.
Timu moja ya Tanzania bara, Azam fc jana usiku iliaga mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 3-0 na Al Merrikh ya Sudan katika mchezo wa marudiano uliofanyika mjini Khartoum.
Kipute cha kwanza Azam Complex, Azam walishinda 2-0.
Wawakilishi wengine wa Tanzania kutoa Visiwani, KMKM walishinda 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan, lakini walitupwa nje kwasababu walipigwa 2-0 Sudan. Wastani ni mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment