Monday, March 2, 2015

YANGA SC wametua jana Dar es salaam majira ya saa 2:00 wakitokea Gaborone, Botswana na moja kwa moja wakaenda kuweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mechi ya keshokutwa dhidi ya JKT Ruvu na mechi ya jumapili dhidi ya Simba SC.
Wakiwa huko walifungwa 2-1 na BDF XI katika mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho iliyopigwa ijumaa iliyopita, lakini Yanga wamesonga mbele kwa wastani wa magoli 3-0, kwasababu februari 14 mwaka huu uwanja wa Taifa walishinda 2-0.
Simba wao wametua jana Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mechi ya watani wa jadi uwanja wa Taifa.
Wataingia katika mechi ya jumapili wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa magoli 5-0 waliovuna juzi uwanja wa Taifa dhidi ya timu vibonge, Tanzania Prisons.
Mkakati ya mechi ya jumapili imeanza kwa pande zote. Kama unavyojua, Simba na Yanga ni mechi yenye mambo mengi, vituko, fitina, mizengwe, lengo ni kwa kila mmoja kuibuka na ushindi.
Mechi ya aina hii inawaletea shida watu wengi, wachezaji, makocha na viongozi, hata mashabiki pia ambao huzimia uwanjani na kupata taabu nyingi kwasababu ya mapenzi yao juu ya timu hizi.
Simba na Yanga wamekuwa katika nafasi tofauti. Wanajangwani wana pointi 31 kileleni, Simba wapo nafasi ya nne kwa pointi 23. Tofauti ya pointi ni 8.
Msimu huu Yanga wamekuwa na mafanikio ya uwanjani kuliko Simba, lakini hicho si kigezo cha kusema Yanga watashinda jumapili, machi 8 mwaka huu.
Simba mbovu alishawahi kuibania Simba bora, Yanga mbovu ilishawahi kuibania Simba bora mara nyingi tu. Mechi za Simba na Yanga si za kuweka rehani vitu vyako.
Maandalizi ya mechi hii ni ya aina yake, watu kuwekewa ulinzi mkali kambini kawaida, wachezaji kupokonywa Simu kawaida, watu kutoingia vyumbani kawaida tu, yote haya yanafanyika kwasababu ushindi una thamani kubwa katika mechi hii.
Simba wanasikika wakisema hata tufungwe na Kagera Sugar,Mbeya City, Stand United, lakini kwa Yanga hatukubali. Sasa wamekimbilia Zanzibar.
Yanga wanachagizwa na ushindi wa 3-0 dhidi ya Prisons, 3-1 dhidi ya Mbeya City fc, halafu wamewakalisha BDF XI.
Kitu kimoja kinachonifurahisha kuelekea mechi ya jumapili:
Kocha na viongozi wa Simba wanadai wanaijenga timu. Juzi mtandao huu umemkariri kocha mkuu, Goran Kopunovic akisema kikosi chake ni kichanga mno, kinahitaji muda, hahitaji miaka 10, lakini anahitaji muda wa kuijenga timu.
Kopunovic anapiga hesabu za mafanikio msimu ujao.
Mserbia huyo anamaanisha hana wachezaji wengi wa kazi, kikosi chake kimejaa vijana wasiokuwa na uzoefu lakini wana vipaji, wengi wanaendelea kujifunza. Ukiwatoa wachezaji kama Ivo Mapunda, Juuko Mursheed, Emmnauel Okwi, Danny Sserunkuma, Saimon Sserunkuma, Masoud Nassor 'Cholo', Simba imajaa vijana wengi waliotokea Simba B.
Kwa upande wa Yanga, kocha mkuu na viongozi, wanaamini wana timu ya ubingwa. Hakuna wachezaji wa kujifunza, asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni wale watu wa kazi, muda wa kujifunza ulishapita, sasa wanacheza mpira.
Nyota kama Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Danny Mrwanda, Mrisho Ngassa, Amissi Tambwe na wengineo hawana tena muda wa kujifunza mpira kama ilivyo kwa Said Ndemla, Mohammed Hussein 'Tshabalala'.
Lakini kumbuka mechi ya 'Nani Mtani Jembe' mwezi desemba mwaka jana Simba ikishinda 2-0. Ni vijana hawahawa walioiadhibu Yanga iliyosheheni nyota wenye uzoefu.
Uchanga wa wachezaji wa Simba sio kigezo cha Yanga kushinda. Mechi hii inakuwa na mambo mengi, wachezaji wanaandaliwa mno.
Kikikosi cha ubingwa v kikosi cha Darasani, nani atatisha?
Nasema kikosi cha Simba ni cha darasani kwasababu kocha anasema wachezaji wake wanaendelea kujifunza na hawana uzoefu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video