Monday, March 2, 2015

Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ujerumani Toni Kroos amesisitiza kuwa ameridhishwa na nafasi anayoicheza kwa sasa na miamba ya soka ya nchini uhispania klabu ya Real Madrid chini ya kocha Carlo Anceloti.

Kroos mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Real Madrid akitokea nchini Ujerumani alipokuwa anakipiga na miamba ya soka nchini humo Beyern Munich msimu uliopita na amekuwa mtu muhimu sana katika kikosi cha kwanza hususani katika safu ya kiungo.
 
Baada ya kulazimishwa sare katika mchezo uliopita wa ligi kuu nchini uhispania na manyambizi Villareal,Kroos aliuambia mtandao wa kijamii wa shirikisho la soka duniani Fifa kuwa wameshazoea mfumo wa kucheza viungo watatu wakabaji katika kikosi cha Anceloti na anafuraha kucheza katika nafasi hiyo kwani yeye sio mshambuliaji bali ni kiungo mkabaji.


"Tangu nilipojiunga na Real madrid msimu uliopita nimekuwa nikicheza nafasi ya kiungo mkabaji na sio mshambuliaji na nina furaha kucheza katika nafasi hiyo kwani ni maamuzi ya kocha kunipanga katika nafasi hiyo, sasa nashangaa mashabiki wakinilaumu kwa kutoshambulia timu pinzani kitu ambacho siwezi kama kiungo mkabaji," alisema Kroos.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video