.jpg)
YANGA SC imeanza vizuri michuano ya kombe la
Shirikisho barani Afrika kufuatia kuichapa mabao 2-0 BDF XI ya Botswana katika
mchezo wa kwanza wa raundi ya awali uliomalizika jioni hii uwanja wa Taifa,
jijini Dar es salaam.
Mabingwa hao mara 24 wa Tanzania walianza mechi
hiyo kwa kuonesha kandanda safi na katika dakika ya kwanza ya mchezo waliandika
bao la kuongoza kupitia kwa Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga kwa kichwa akimalizia
mpira wa kona wa winga machachari, Simon Msuva.
Tambwe aliyekuwa na umakini leo alitia kambani bao
la pili dakika ya 55’ kwa njia ya kichwa akimalizia krosi ya Mrisho Khalfan
Ngassa.
Katika vipindi vyote viwili, Yanga walitawala
mchezo wakicheza pasi nyingi, lakini walishindwa kutengeneza nafasi nyingi za
kufun
Hata hivyo Yanga waliendelea kupoteza baadhi ya
nafasi walizopata na wangekuwa makini wangepata ushindi mkubwa zaidi.
Kikubwa walichofanikiwa BDF XI ni kucheza mpira wa
kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza.
Malengo yao yalikuwa kukwepa kichapo kikubwa ili
wakajipange upya nyumbani na ndio utamaduni wa michuano mikubwa barani Afrika.
Kitu wanachotakiwa kujirekebisha Yanga ni kucheza
mpira wa pasi wenye madhara, kwasababu wanajikuta wakigongeana pasio nyingi
katika eneo lao na kushindwa kuisogeza timu na kulazimisha mashambulizi.
Mechi ya nyumbani lazima utumie mbinu nyingi
kufika langoni kwa mpinzani hata kama anacheza soka la kujihami zaidi.
Yanga wanastahili pongezi kwa ushindi huo waliopata kwasababu BDF wanahitaji ushindi wa mabao 3-0 ili kuwatupa nje Yanga.
Kwa upande wa Yanga wanahitaji kufungwa bao 1-0 au sare ya 1-1 ili kusonga mbele na kwa uwezo waliokuwa nao Wanajangwani wanaweza kushinda.
Kikubwa ni kuongeza nidhamu hasa katika kutumia nafasi wanazopata na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Baada ya Yanga, kesho uwanja wa Azam Complex, Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc watachuana na mabingwa wa Sudan, EL Merreick katika mechi ya raundi ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment