
KIUNGO wa Manchester United, Juan Mata ameingia katika rada za usajili za Barcelona kwa mwaka 2016 na tayari miamba hiyo ya Katalunya imeshaanza mipango ya usajili kwa mwaka ujao.
Kikosi cha Luis Enrique bado kinatumikia kifungo cha kutosajili walichopewa na FIFA baada ya kuvunja sheria za uhamisho kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18.
Kwa mwaka 2015 Barcelona hawatakiwi kusaini mchezaji yeyote, lakini Mata ambaye hana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha Van Gaal anahusishwa kujiunga na miamba hiyo ya Nou Camp, kwa mujibu wa gazeti la Hispania la Mundo Deportivo.
0 comments:
Post a Comment