SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF, limefanyia
marekebisho ratiba ya ligi kuu Tanzania bara sambamba na mechi za viporo.
Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotumwa kwa vyombo
vya habari leo, alhamisi ya wiki hii (februari 19 mwaka huu) kutakuwa na mechi mbili za viporo.
Tanzania Prisons watachuana na Yanga katika mechi
ya kiporo uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya, wakati Azam fc wataikaribisha Ruvu
Shootings ya Pwani katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex.
Mwishoni mwa wiki hii, jumamosi ya februari 21 na jumapili
februari 22 mwaka huu mechi kadhaa zitapigwa viwanja mbalimbali.
Jumamosi, Kagera Sugar watachuana na Polisi
Morogoro uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, wakati Ndanda fc watamenyana na
Coastal Union dimba la Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mgambo JKT itapepetana na Mtibwa Sugar uwanja wa
CCM Mkwakwani Tanga.
Jumapili; Stand United watatifuana na Simba uwanja
wa Kambarage, wakati Azam fc watashuka dimbani dhidi ya Tanzania Prisons, mechi
hii itapigwa usiku uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Yanga ya Dar es Salaam itashuka dimbani ugenini kukabiliana
na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine.
MECHI ZA VIPORO
Februari 22, 2014, Mbeya City fc v Yanga, uwanja
wa Sokoine
Machi 18, 2015, Mtibwa Sugar v Tanzania Prisons , uwanja
wa Manungu.
Tutaendelea kukujuza ratiba nzima kadri mechi
zinavyochezwa….

0 comments:
Post a Comment