
MABAO mawili ya Cristiano Ronaldo na Marcelo yametosha kuwapa ushindi wa mabao 2-0 Real Madrid dhidi ya Schalke 04 katika mechi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya iliyopigwa uwanja wa Veltins Arena, Ujerumani.
Ronaldo aliifungia Real bao la kuongoza katika dakika ya 26' kipindi cha kwanza na Marcelo alitia kambani bao la pili na la ushindi katika dakika ya 79'.

Real Madrid walitawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa na mpaka dakika 90 zinamalizika waliongoza umiliki wa mpira wa asilimia 61 dhidi ya 39 za Wajerumani.
Lichaya kumiliki mpira, hawakuweza kufika mara nyingi zaidi kwa wapinzani wao kwani walifanikiwa kupiga mashuti 4 yaliyolenga lango sawa na wapinzani wao.
Timu zote zilipiga kuona 2, wakati huo huo Real Madrid waliotea mara 3 na Schalke mara 1. Hii inaonesha wenyeji walifika mara chache zaidi katika eneo la wageni wao.

Kutokana na kuzidiwa zaidi, Schalke waliwafanyia madhambi mara 15 wachezaji wa Real, wakati wakali hao wa Santiago Bernabea walifanya madhambi mara 9.
Kutokana na makosa, Schalke walioneshwa kadi 3 za njano na Real 1.
Kwa matokeo hayo, Real wanahitaji sare ya aina yoyote au kufungwa goli 1-0 nyumbani ili wasonge mbele hatua ya robo fainali.

Katika mechi nyingine Basel ya Uswizi iliikaribisha FC Port ya Ureno na mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1.
Bao la mapema la dakika ya 11' la Derlis Gonzalez liliwafanya Basel waongoza, lakini dakika ya 79' Danilo alifuta goli hilo kwa mkwaju wa penalti.
Hata hivyo Porto walicheza mpira wa kiwango cha juu na walitawala kwa asilimia 61 kwa 39.
Walipiga mashuti 7 yaliyolenga lango, wakati Basel walipiga hawakupiga shuti 1.
Wageni walipiga kona 9 wakati wenyeji hawakuiga kona yoyote.
FC Borto wanahitaji suluhu (0-0) au ushindi wa aina yoyote katika mechi ya marudiano ili kutinga robo fainali.
0 comments:
Post a Comment