
KWANINI kila mtu alishangaa? Hii ni kwasababu Cristiano Ronaldo amemaliza maneno juu ya ukame wa kutofunga magoli aliokuwa anakabiliwa nao baada ya jana kufunga goli la 58 katika michuano ya ligi ya mabingwa akiicheza Real Madrid katika ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya kikosi cha Schalke 04 kinachonolewa na kocha aliyewapa ubingwa pekee wa UEFA, Chelsea, Roberto Di Matteo.

Mbali na kufunga, pia alimtengenezea nafasi ya kufunga Marcelo aliyetia kambani bao la pili kipindi cha pili.
Ronaldo hakufunga katika mechi tatu alizocheza kabla ya jana.
Huko nyuma hakuwahi kucheza mechi 4 bila kufunga ndani ya miaka minne, lakini jana alipiga kichwa murua kilichomzidi kipa kinda mwenye miaka 19 Timon Wellenreuther na kuwafanya Real Madrid kuwa mbele kwa bao 1-0 kipindi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment