Sunday, February 22, 2015

YANGA na Azam fc zinachuana kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanznaia bara.
Kwasasa kikosi cha Hans van der Pluijm kipo kileleni kwa pointi 28, kikiwa kimeshuka dimbani mara 14.
Kimeshinda mechi 8, sare 4 na kupoteza 2. Kimefunga mabao 18n na kufungwa 7, tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ni 11.
Azam fc wanashika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 26 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Wanalambalamba hao wamefunga magoli 22 na kufungwa 12, tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ni 10.
Endapo Azam wanahitaji kurudi keleleni wanahitaji kuiombea Yanga mabaya ili ipoteze mechi ya leo dhidi ya Mbeya City fc na wao washinde. Au Yanga itoke suluhu (0-0) na wao washinde 2-0.
Kama Yanga watatoka suluhu, watafikisha pointi 29, lakini mabao yatabaki yale yale niliyoeleza hapo juu. Azam wakishinda 2-0 watafikisha pointi 29 sawa na Yanga, lakini idadi ya mabao ya kufunga itakuwa 24, ya kufungwa 12, wastani utakuwa 12. Bao moja zaidi ya Yanga. Hivyo watarudi kileleni.
Usiku wa leo Azam fc wanachuana na Prisons katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Hii ni mechi ya pili ya ligi kuu kuchezwa uwanja wa Azam Complex usiku, kwani JKT Ruvu na Ruvu Shooting walichuana mwaka jana.
Azam wamekuwa na rekodi nzuri katika uwanja wao, kabla ya kuivaa Al Merreick, katikati ya wiki iliyopita waliwachapa 5-2 Mtibwa Sugar na wakawachapa wakali wa Sudan 2-0 ligi ya mabingwa.
Kwa namna Prisons wanavyoungaunga maisha, wanaweza kuchapwa goli nyingi, ingawa sio lazima iwe hivyo.
Mbeya City na Yanga ni mechi ngumu. Mwaka jana zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Sokoine na leo mechi itakuwa ngumu na lolote linaweza kutokea.
Mechi nyingine kubwa inachezwa jioni ya leo uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga baina ya wenyeji Stand United dhidi ya Simba.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video