Cholo (kulia) alikosa penalti dhidi ya Mbeya City fc na kuanzia siku hiyo hajacheza tena na nafasi yake imeshikiliwa kwa muda mrefu na Hassan Ramadhani Kessy
BEKI mkongwe wa kulia na nahodha wa zamani wa Simba, Masoud Nassor Cholo amesema: "Simba ni timu yetu wote, inapofanya vibaya wachezaji, viongozi, wanachama na mashabiki tunaumia sana".
"Kikubwa tuungane, kwa upande wetu tunajitahidi kufanya vizuri, kocha ni mzuri, tunaimarika kila siku. Tumeshinda 2-0 ugenini wiki iliyopita, leo tunahitaji ushindi dhidi ya Stand United".
"Mechi ni ngumu, Stand ni wazuri, lakini tumejianda kwa ushindi".
Stand United United wanaikaribisha Simba katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara leo jioni.
0 comments:
Post a Comment