Nahodha wa klabu Chelsea John Terry amesema
anataka kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi huku akiomba uongozi wa klabu kumuongezea miezi 12 katika Mkataba
wake mpya.
Terry ambaye ni beki wa kati katika kikosi cha Mreno Jose Mourinho, ana umri wa miaka 34, Na Mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, akiwa ameichezea Chelsea the blues michezo 656 katika dimba la Staford Bridge.
Mchezaji huyo Raia wa Uingereza alisema kwa kiwango alichonacho kwa sasa anaamini klabu hiyo inafahamu nafasi yake katika klabu na itafikilia kuendelea kumbakiza Stanford Bridge kuitumikia klabu hiyo.
"Timu inafahamu nafasi yangu ninataka kusalia Stanford Bridge, na naamini kiwango changu kinaonesha wanaweza kunibakisha",Alisema Terry.
Terry alianza kuitumikia Chelsea mwezi Oktoba mwaka 1998 mpaka sasa mwaka 2015 bado yupo na miamba hao wa soka wa nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment