
Anatazama mbele: Wayne Rooney amesema wachezaji wa England wako nyuma ya kocha wao Roy Hodgson
NAHODHA wa England Wayne Rooney amedai wachezaji wa Simba watatu kwa asilimia 100 wapo nyuma ya kocha Roy Hodgson kuelekea mchezo wa leo wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Uswizi.
Hodgson amepoteza mvuto kwa mashabiki wa England kufuatia kufanya vibaya katika fainali za kombe la dunia na anakabiliwa na presha kubwa ya kusaka ushindi mbele ya Uswizi inayokuja juu katika medani ya soka.
Mechi hiyo muhimu kwa England itapigwa katika dimba la St Jakob Park usiku wa leo.
Pia meneja huyo wa England anatoka jasho kutokana na kutokuwa fiti kwa kiungo wake Jordan Henderson ambaye alitolewa nje wakati wa mazoezi ya jana usiku baada ya kupata majeruhi katika mguu wa kulia.
Hodgson alitarajia kumpanga Henderson na Jack Wilshere katika safu ya kiungo.
James Milner atachukua nafasi ya Henderson kama atashindwa kuimarika.

Kiti cha moto: Hodgson amekuwa akikosolewa baada ya kuvurunda katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika majira ya kiangazi nchini Brazil
Wasiwasi: Jordan Henderson anaweza kukosa mechi ya kuwania kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswizi leo usiku.
0 comments:
Post a Comment