Shida tena: Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli akijibizana na mwamuzi Chris Foy
MSHAMBULAIJI wa Liverpool , Mario Balotelli alitolewa uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Wolves baada ya kurushiana maneno na mwamuzi Chris Foy.
Katika mechi hiyo, Liverpool walishinda bao 1-0.
Nyota huyo mwenye miaka 24 aliyejiunga Anfield akitokea AC Milan kwa dau la paundi milioni 16 mwezi uliopita, alionekana kutulizwa na Kolo Toure wakati Foy akijaribu kujibizana naye katika dimba la Melwood.
Inafahamika kuwa Muitaliano huyo alikuwa anachuana katika mpira wa 50-50 na mchezaji wa Wolves.
Hakuna kilichotokeo baada ya tukio lile zaidi ya Balotelli kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine.
Hakuna furaha: Kolo Toure (kushoto) akimshika Balotelli
Unakwenda benchi! Balotelli akienda benchi dakika chache baada ya tukio hilo

0 comments:
Post a Comment