Majeruhi tena: Diego Costa hana jinsi zaidi ya kuondolewa katika kikosi cha Hispania kitakachochuana na Macedonia
MSHAMBULIAJI hatari wa Chelsea, Diego Costa ametemwa katika kikosi cha Hispania kitakachopambana na Macedonia kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 kutokana na kupata majeruhi ya nyama za paja.
Nyota huyo tegemeo kwa Jose Mourinho amepata tatizo linalofanana na lile alilopata miezi minne iliyopita na alilazimika kutoka katika mechi ya kirafiki ya Hispania dhidi ya Ufaransa jana alhamisi baada ya kuhisi maumivu.
Munir El Haddadi, nyota anayekuja juu katika klabu ya Barcelona atachukua nafasi ya Costa katika mchezo wa jumatatu mjini Valencia.
Walitandikwa: Hispania walitandikwa bao 1-0 na Ufaransa katika mechi ya kirafiki uwanja wa Stade de France jana usiku.

0 comments:
Post a Comment