Uwanja mbaya: Gareth Bale alisema dimba la 3G huko Andorra ni baya zaidi kulivyo licha ya kufunga mabao mawili na kuipa Wales ushindi.
TIMU ya Taifa ya Wales umefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ngeni ya Andorra katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2016.
Bao pekee la Andorra lilifungwa na Ildefons Lima , wakati mawili ya Wales yalifungwa na Gareth Bale.
Hata hivyo, Bale amedai kuwa uwanja wenye nyasi za bandia wa Andorra Estadi Nacional ni mbovu zaidi kuliko viwanja vyote vibovu alivyowahi kucheza.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa pichi la 3G kutumika katika mechi na ugumu ulikuwa katika umilikaji wa mpira.
Mkombozi: Licha ya ushindi, Bale amedai uwanja ulikuwa kikwaza kikubwa
Aliwindwa: Bale alikumbana na upinzani mkali kwa mabeki wa Anorra ambao hawakuwa na mchezo naye

0 comments:
Post a Comment