Maumivu: Aaron Ramsey alipata majeruhi ya kifundo cha mguu
AARON Ramsey yuko hatarini kukosa mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City siku ya jumamosi baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa Wales wa mabao 2-1 dhidi ya Andorra jana usiku.
Kiungo huyo alipata majeruhi hayo baada ya kufanyiwa rafu na mchezaji wa Andorra ambapo alipatiwa matibabu, lakini akatolewa uwanjani.
Meneja wa timu, Chris Coleman alisema ukubwa wa majeruhi utatangazwa saa 24 kuanzia jana usiku, na hali hiyo imempa maumivu ya kichwa, kocha Arsene Wenger.
Akianguka chini: Ramsey alipata majeruhi ya kifundo cha mguu akichuana na mchezaji wa Andorra.
Majanga: Daktari wa Wales akimsaidia Ramsey, lakini alishindwa kuendelea na mechi
Alitweet: Chris Coleman alisema anaamini majeruhi ya Ramsey haiwezi kumuweka nje ya uwanja wa muda mrefu

0 comments:
Post a Comment