Tuesday, September 9, 2014

 
 BENKI ya Exim  Tanzania imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Stand United inayojiandaa kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.

Stand United yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga itaanza kampeni zake nyumbani kwa kuvaana na wageni wenzao wa ligi kuu, Ndanda fc kutoka Mtwara.

Taarifa zinaeleza kuwa katika mkataba hao, Stand United watalamba milioni 10 za Kitanzania.

Huu ni udhamini wa nne kwa klabu hiyo kwani tayari walishalamba udhamini wa kampuni ya Binslum sambamba na klabu za Mbeya City na Ndanda fc ya Mtwara ,Azam Tv na wadhamini wakuu wa ligi, kampuni ya Simu za mkononi, Vodacom Tanzania.

Kwa maana hiyo, Stand United watakuwa wanakusanya fedha za udhamini kutoka Binslum, Azam TV na Benki ya Exim.

Mkataba wa Exim na Stand United unahusisha kuweka  mabango ya benki hiyo  uwanjani, nembo kwenye gari la timu na kwenye jezi. Pia kuweka bango nyuma ya mikutano ya viongozi au makocha wakati wanazungumza na waandishi wa habari.

Hivi karibuni wachezaji wa Stand United waliripotiwa kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara, lakini uongozi ukafafanua kuwa kuna mahali kulitokea tatizo na fedha zipo.

Viongozi hao walikiri kufanya uzembe na walifanikiwa kumaliza tatizo.

Kwa udhamini huu, Stand United watakuwa na uwezo wa kufanya mambo ya msingi klabu kwao.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video