
Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 1:07 usiku
JOSE Mourinho
amekuwa akikosolewa kwa kumuacha mshambuliaji kijana kuondoka Chelsea, lakini
Pete Hall anasema The Blues wamepata doa.
Baada ya kushika
nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa ligi kuu msimu uliopita (nyuma ya
Robin van Perise na Luis Suarez), watu wengi wamekuwa na maswali kuwa ni kitu
gani Lukaku angefanya ili kupata nafasi ya kucheza Chelsea.
Kufunga zaidi ya
mabao 10 kwa msimu ni kitu ambacho Diego Costa aliyesajiliwa amefanya mara
moja, wakati Lukaku amefunga mabao kama hayo mara nne licha ya kutoaminiwa
katika maisha yake ya soka.
Akiwa ameichezea
Chelsea ligi kuu kwa dakika 199 tu tangu ajiunge miaka mitatu iliyopita kutokea
Anderlecht, ilikuwa rahisi kwa klabu hiyo ya London Magharibi kumuuza baada ya
dau la paundi milioni 28 kuwekwa mezani.
PESA NDIO MUHIMU
Kama sehemu ya
kuweka sawa mahesabu wakati huu wa sheria ya matumizi ya fedha kwa Chelsea.
Jose Mourinho hajaona tatizo kumuuza nyota kijana anayechipukia. Anajua wazi
kuwa kuendelea kumlipa hela mchezaji asiyemtumia ni hasara kuliko kumuuza moja
kwa moja.

“Ni kijana mdogo
anayependa kuzungumza. Lakini kitu pekee ambacho hakusema ni kwanini alienda
kwa mkopo Everton,” Mourinho alisema mwezi desemba alipokuwa anazungumzia
hatima ya Mbelgiji huyo.
Imeaminika kuwa Mreno
huyo hana nia ya dhati kwa vijana baada ya kumuuza Lukaku na kumuacha Fernando
Torres licha ya kufunga kwa asilimia 13.51 kwa nafasi alizopata misimu miwili iliyopita.
Mabao 71 ya Chelsea
msimu uliopita yalikuwa machache zaidi ukilinganisha na ya mabingwa watetezi
Manchester City, lakini Costa ameletwa kumaliza tatizo hilo akiwa amafunga
mabao 27 na Atletico Madrid msimu uliopita na kuisaidia kutwaa ubingwa wa La
Liga.
HAKI YA KUUZA
Wakati mjadala
unaendelea kama Mourinho atajuta kumuuza nyota huyo, klabu imenufaika na dau
walilopata katika mauzo ya Lukaku.
Paundi milioni 50
walizotumia misimi miwili iliyopita zimejaribu kupunguzwa. Shukurani kwa Mourinho kwa kumsajili Diego Costa, Filipe
Luis na Cesc Fabregas.
Ukilinganisha na
wapinzani wao Manchester United ambao walilundika paundi milioni 112 kwa miaka
miwili iliyopita, ilikuwa faida sana kwa kulinganisha na matumizi makubwa ya
Chelsea katika soko la usajili.
Asernal licha ya
kulaumiwa na mashabiki wake kutosajili, ilitumia paundi milioni 92 ndani ya
miaka miwili iliyopita.

Juan Mata naye aliachiwa na kuondoka Chelsea
Wakati huo huo,
vikwazo alivyowekewa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour baada ya kutumia
fedha nyingi katika usajili kinyume na sheria ya matumizi ya fedha, inaonekana kuwaogopesha
wengi.
Mourinho aliogopa
zaidi kwasababu baada ya kumsajili Drogba, alibakiwa na nafasi moja ya mchezaji
wa kigeni.
“Nahitaji kuuza
mmoja,” bosi huyo wa Chelsea alisema wiki iliyopita. “Kama unadhani wote
wanatakiwa kubakia, hauko sahihi. Mmoja lazima aondoke”.
Kuondoka kwa Lukaku
sio tatizo sana. Kwa kuwa kuna viungo washambuliaji wengi Chelsea , timu inaweza
kufanya vizuri kuliko hata Asernal, na hata kama Costa atashindwa kufanikiwa
kama anavyotabiriwa na watu wengi, klabu hii inaweza kufanikiwa.
UKWELI WA KUUZWA
KWA LULAKU
Kiukweli, Chelsea
haina mashabiki wengi na biashara ya kuzalisha fedha kama ilivyo kwa Manchester
United. Kwa hiyo kumuuza Lukaku ambaye hakuwa kwenye mipango ni bora kuliko
kumbakiza.
Katika ulimwengu wa
soka, ukiona klabu inamuuza mchezaji mwenye umri mdogo aliyefunga mabao mengi
akiwa na miaka 21 ambayo hata Lionel Messi hakuwahi kufunga wakati wa umri huo,
basi ujue ni masuala ya fedha na biashara.
Mwisho wa siku,
Jose Mourinho anajua anachokifanya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment